BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Friday, July 10, 2009

HII NDIO TANGA CITY- KWA WALE WASIOIJUA VIZURI!!!


Hapa maeneo yaTunakopesha Ltd, kama unaelekea Tanesco!




Hapa ni stendi ya mabasi ya mikoani, tazama mabasi yanavyong'ara huku watu wakipita




Eneo hili ni nyuma ya Club maarufu jijini Tanga Lacasa Chica. Lakini ukisogea kwa mbele utakutana na jengo la TTCL na jengo la Benki ya Posta.


Hili ni jengo maarufu kwa kukodisha ofisi. Humo kuna ofisi nyingi- jengo hili linatazamana na jengo la Nasaco karibu na hoteli ya Meridian



Hapa ni makutano ya barabara ya kwenye hospitali ya Bombo na Bandari ukiwa unatokea maeneo ya Tanesco.

Ushawahi kusikia zile barabara za namba, yaani kuanzia moja hadi ishirini..? Basi hii ni Taifa Road lakini ikiwa ni barabara ya 12 jijini Tanga.


Huku ni maeneo kama unaelekea Splendid Hotel, moja kati ya hotel maarufu jijini Tanga.



Hilo jengo la rangi ya pinki, ni jengo la Benki ya Exim. Moja kati ya benki zinazotoa huduma nzuri.



Maeneo ya jengo la TTCL likiwa limepakana na jengo la chuo cha Engusero hapa jijini Tanga.



Jamani eeh, hili ni moja kati ya majengo maarufu Tanga. Lipo maeneo ya Four Ways. Kuna huduma nyingi za kijamii zinatolewa hapo.



Hi ni clock tower ambayo ipo maeneo ya Chumbageni kama unaelekea Chuda Raha.



Hili ni jengo la Toyota, kama unahitaji magari ya aina hiyo utayapata jijini Tanga pia. Uliposikia Tanga ni jiji, sio masihara mdau!!




Makutano ya barabara ya Tanesco kwa magari yanayofanya mizunguko ya mji kuelekea Raskazoni.



Hili ni jengo la Benki ya Baclays hapa jijini Tanga. Moja kati ya mabenki ambayo yameamua kutoa huduma zake kwa wakazi wa hapa.




Stendi tena, tazama dada na ushungi wake akikatiza mitaaa!!



Kwa wale wapenda starehe, naweza kusema MAMBO IKO HUKU!!! Jengo la klabu Lacasa Chica- Club maarufu jijini Tanga kwa starehe. Wasanii wote wa muziki hufikia hapa kwa ajili ya kukonga nyoyo za wapenda raha- TANGA RAHA!!!



Maeneo ya Four Ways, hili pia ni jengo ambalo kwa hakika linatia fora. Kwa pembeni kama unaelekea barabara hiyo, kuna bonge moja ya Bar maarufu sana kwa nyama choma!!


Tazama bustani zilivyonakshiwa vizuri. Hili jengo linatazamana
na viwanja vya Tangamano ambavyo ni maarufu sana kwa soko huria.



Jamani...hii yote ni Tanga. So enjoy ili na wewe siku moja uje kupaona!



Jengo refu kuliko yote jijini Tanga la Bandari, ambalo kwa hakika ni moja kati ya vivutio. Ukipanda jengo hili utaiona Tanga nzima, na pia kwa upande wa pili utaiona bahari ya Hindi ambayo watu wa Tanga pia tumebarikiwa.


Next time nitawawekea picha za vivutio vya asili ambavyo vipo Tanga kama mapango ya ambaoni n.k.- Hii ni zawadi kwa wadau wangu popote pale mlipo. Karibuni Tanga jamani, tule raha na kufurahia upepo wa pwani!!!



No comments:

Post a Comment