BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Monday, August 17, 2009

SHOW YA TMK FAMILY NA TIP TOP CONNECTION JIJINI TANGA- AIBU TUPUUU!!! (PART ONE)



Meneja wa kundi la Tip Top Connection Hamisi Tale maarufu kama Babu Tale akipiga msosi, kabla ya show kuanza

Nae raisi wa Manzese- Madee akipiga menyu kali katika kuhakikisha anakamua ipasavyo stejini
Mkubwa Fela pamoja na Tunda Man wakiteta jambo kwenye hoteli waliyokuwa wanapata chakula mchana wa jana kabla ya show

Hapa nje ya uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga- watu wakiwa kwenye foleni ya kukata tiketi kwa ajili ya kuinghia ndani.

Show ilichelewa kuanza- na hata ilipoanza ilikuwa tayari watu wameshachoka. TMK ndio walioanza kutoa burudani.


Kilichowashangaza watu wengi ni kwamba, hakukuwa na STEJI hivyo wasanii wote kulazimika kufanya show kwenye vumbi.



Pamoja na kupiga show kwenye VUMBI lakini Wanaume walipiga mzigo hivyo hivyo huku Chege Na Temba wakionekana kuokoa jahazi.

Dah mdau usipimeee!! ilikuwa noma- wasanii walikuwa wanaimba huku wakiwa na nyuso za huzuni kutokana na kutofurahia mazingira yale ya vumbi. Ilikuwa kama tupo kwenye hizi disko za mitaani maarufu kama DISKO VUMBI!


Miguu ya msanii maarufu nchini Cassim kama inavyoonekana katika picha ikiserebuka
Tunda Man alikuja baadae sana nae kuokoa jahazi- hata hivyo alipigiwa shangwe alipoimba wimbo wa Nipe Ripoti na Neila


Zantel nao walikuwepo kutoa sapoti kwa CHAMA KUBWA!!


Bra-A aliyevaa kikoti na Anko Mo kutoka redio Mwambao wakiwa na msanii Keisha

Ilipigi Mkubwa Fela amsimamie Dj kutokana na mauvundo aliyokuwa akiyafanya




Keisha aliimba wimbo mmoja tu wa Uvumilivu aliomshirikisha Squizer- kushoto aliyevaa kofia na kitambaa ni Abdu Bonge wa Tip Top.
Pamoja na kukosekana kwa Steji- jamani hata TAA pia hazikuwepo. Uwanja mzima ulikuwa kiza- wasanii walifanya show kwenye vumbi huku wakimulikwa na taa za magari matatu yaliyokuwa yamewasha taa za mbele.
Kwa upande fulani, show ilikuwa kama yakulazimasha sanaaaa! Coz tayari watu ndio wameshaingia, pesa wameshatoa- kurudisha itakuwa ngumu na wakati huo huo hakuna STAGE hakuna TAA. Ikabidi iwe hivyo hivyo bora liende ili kuepusha shari.


Kutoka Da Hot Beat Show ya Mwambao Fm Redio jijini Tanga: Bra-A, Moshen Habib na mtu mzima Anko Mo wakifuatilia show ya Chama Kubwa kwa makini.


TMK Wanaume Familiy na Tip Top Connection wapo kwenye ziara mikoani kutambulisha albamu tatu kwa pamoja ambazo ni FELA NA WANAWE ya kwakwe Mkubwa Fela- PESA YA Madee na Mtoto wa Kichaga ya Mh. Temba.
Kama kuna mikoa ambayo tayari wamepita na kufanya show- basi hii ni show yao ya kwanza kuharibu hapa Tanga. Kama una maoni kuhusiana na show hii niandikie kupitia E-mail yangu ambayo ni
ankomo25@yahoo.com MAONI YOTE NITAYAWEKA HAPA HAPA!!
Hii ni Part One jamani-




Wednesday, August 12, 2009

KONGAMANO LA WANABLOG LINAKUJA TANZANIA!!


Je wewe ni mwanablogu (Blogger) au mdau wa habari na mawasiliano kwa umma kwa kutumia mtandao? Kama jibu ni ndio, tafadhali unaombwa kujiorodhesha kwa ajili ya maandalizi ya Kongamano Maalumu la Kitaifa kwa ajili Wanablogu (Bloggers) na wadau wa habari na mawasiliano wa Tanzania (Tanzanians Bloggers Summit) linalotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu jijini Dar-es-salaam,Tanzania.

Dhumuni la kongamano hili ni Kuelimishana, Kufahamiana, Kuamsha Utambuzi Rasmi Kuhusu Tekinolojia ya Blogu na Mawasiliano ya Umma kwa Kutumia Mitandao, Kusaidia Utambuzi Rasmi juu ya mchango wa blogu nchini Tanzania kama chombo muhimu cha habari na mawasiliano, Kuelimishana jinsi gani blogu zinaweza kutumika katika kuleta maendeleo katika nyanja za kijamii, kisiasa na kiuchumi, kuburudisha, kukuza utamaduni nk.

Wataalamu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wataalikwa kutoa mada na mafunzo mbalimbali kuhusiana na tekinolojia ya kublogu, zana nyinginezo za mawasiliano mtandaoni kama vile mitandao jamii(social networking), online forums nk.Kutakuwa na vipindi vya maswali na majibu.
Ili kufanikisha maandalizi ya Kongamano hili la kihistoria, kujiorodhesha kwako ni muhimu sana.
Muda wa kujiodhoresha ni kuanzia tarehe 12/8/2009 (Jumatano) mpaka 12/9/2009 (Jumamosi) tu.
Kinachohitajika ili kujiandikisha ni :
Jina Lako, Anuani yako ya barua pepe (E-mail), Mahali Ulipo au unapoishi (Nchi,mji nk),Namba ya Simu (sio lazima) na Anuani au URL(Universal Resource Locator) ya blogu yako (mfano)
www.kongamano.blogspot.com/wordpress.com/.com/typepad nk). Vyeti vya Ushiriki vitatolewa kulingana na habari utakazoziorodhesha hapa.
Unaweza kujiorodhesha kwa kutuma ombi lako kwa barua pepe kwenda; summit@bongocelebrity.com.
Zingatia tarehe za kujiandikisha.
Ni mwezi mmoja tu! Asante kwa ushirikiano.
Kwa mujibu ya bongocelebrity.com
UMOJA NI NGUVU!

Thursday, August 6, 2009

UFAHAMU MKOA WA TANGA, TANZANIA.


UFAHAMU MKOA WA TANGA

Mkoa wa Tanga unapatikana Kaskazini Mashariki mwa nchi ukiwa unapakana kabisa na Bahari ya Hindi. Mkoa huu ambao wenyeji wake ni watu wa makabila ya Wasambaa, Wabondei na Wadigo.

Shughuli kubwa za kiuchumi za wenyeji wa mkoa huu ni za kilimo na uvuvi ambapo shughuli za kilimo hujumuisha uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara, mkonge ukiongoza kama zao la biashara mkoani hapa.

Mkoa wa Tanga unayo idadi ya watu anaofikia 1,642,015 ambao hulijaza eneo la kilometa za mraba 26,808 ambazo ni sawa na maili za mraba zipatazo 10,351.
Mkoa huu unayo majimbo ya uchaguzi yanayofikia (8) ambayo yanajumuisha Kilindi, Tanga Mjini, Handeni, Lushoto, Bumbuli, Muheza, Korogwe Magharibi, Korogwe Mashariki.


MALIASILI

Misitu:
Katika Mkoa wa Tanga zipo hekta 6,000 za mashamba ya miti ya kupanda kwa ajili ya uvunaji – Shume (Lushoto) na Longuza (Wilayani Muheza).

Misitu ya Hifadhi:
Jumla ya hekta 160,795 ni misitu ya hifadhi ya vyanzo vya maji na bioanuwai iliyotengwa sehemu mbalimbali za Mkoa

Wanyamapori:
Mkoa una kilometa za mraba 5,920 kwa ajili ya mapori ya wanyama; ikiwa kati ya eneo hilo, kilometa za mraba 3,120 ni “Game Controlled Areas”.Mkoa pia unachangia katika eneo la Hifadhi ya Taifa ya Saadani yenye ukubwa wa kilometa za mraba 1,062. Aidha, lililokuwa pori la akiba la Umba sasa limekuwa Mbuga ya Taifa ya Wanyama (National park) baada ya kuunganishwa na Pori la Akiba la Mkomazi katika Mkoa wa Kilimanjaro




Monday, August 3, 2009

T.I.D KUTOKA NA FILAMU YAKE YA JELA!!


Khalid Mohammed ‘TID’, anatarajia kuachia filamu yake mpya inayoelezea maisha yake ya jela.

TID aliyabainisha haya hivi majuzi na kusema kuwa anatarajia kurejea katika anga za filamu kwa kishindo.


Akielezea kuhusu filamu hiyo alisema itakuwa ikizungumzia kuhusu kosa alilolifanya na kumfanya apelekwe jela ikiwa ni pamoja na maisha halisi aliyokuwa akiyaishi huko jela.


“Ndoto ya kutoa historia ya maisha yangu jela katika filamu niliipata tangu nikiwa huko jela na nilipofika uraiani nimeamua kuikamilisha,” alisema TID.