BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Wednesday, March 30, 2011

TUNDA MAN, KASSIM NDANI YA TANGA ALHAMISI YA LEO

BASI IMBA- TUNDA MAN FT RICHARD



USIENDE KWA MGANGA- KASSIM



BAN Entertainment na La Grand Lacasa Chica kutokea Tanga City, wanakuletea show ya Mahalat itakayofanyika Alhamisi ya leo ya tarehe 31/03/2011 kunako Club Lacasa Chica.

Show hiyo ya aina yake itawaweka wasanii nguli wa Bongo Flava Kassim Mganga pamoja na Tunda Man. Pia kutakuwa na BAIKOKO LIVE, RUSHA ROHO na MASEBENE ya hatari.

Kiingilio ni 3000/= kwa wanaume na 2000/= kwa wanawake. NYOTE MNAKARIBISHWA.

Monday, March 28, 2011

'PILATO NA GAME'- BWANA MISOSI

"Nakuja na ujio mpya nyimbo inaitwa'Pilato na Game' nimewashirikisha Nature na Fid Q na producer ni Makochali toka Mj recordz,video iko tayari chini ya Kallages picture na wiki la kesho audio na video itakua hewani.." Anaitwa Bswana Misosi msanii maarufu wa muzikiwa wa Bongo Flava kutokea Tanga, Tanzania.

ENDELEA KUJIUNGA NA MARAFIKI WA TANGA!

Ungana na MARAFIKI WA TANGA - BONYEZA HAPA


Hakikisha umefungua facebook yako ili kujiunga.

MOMBO WALIVYOKABIDHIWA GARI LA KUBEBEA WAGONJWA!

Gari la kubebea wagonjwa jipya kabisa lililokabidhiwa uongozi wa kituo cha afya cha Mombo wilayani Korogwe na uongozi wa Hoteli maarufu ya Liverpool iliyopo katika mji huo mdogo wa Mombo.

Mkuu wa mkoa wa Tanga ndie alikuwa mgeni rasmi siku hiyo katika hfla ya kukabidhi gari hilo la wagonjwa. Pichani akijaribu kuliwasha kama ishara ya kulizindua huku mkurugenzi wa hoteli ya Liverpool akiangalia.

Mkuu wa Mkoa na Mukrugenzi wa Liverpool wakipongezana mara baada ya gari hilo kuwa sawa. Watatu kutoka kulia ni mbunge wa Korogwe vijijini PR Maji Marefu.


Thursday, March 24, 2011

'THE MECHANIC'



Je wewe ni mpenzi wa movies za action!!? itafute hii na itakosha nafsi yako

Tuesday, March 22, 2011

MASHINDANO YA SHIMIWI NI OKTOBA JIJINI TANGA

MASHINDANO ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (Shimiwi) mwaka 2011 yamepangwa kuanza Oktoba 13 hadi 30 Tanga. Akizungumza na Blog hii, Katibu Mkuu wa Shimiwi, Ramadhani Sululu alisema michezo hiyo ya kila mwaka inashirikisha wanamichezo wanawake kwa wanaume.

Alisema michezo tisa itashindaniwa katika mashindano hayo ambayo mwaka jana hayakufanyika kutokana na Uchaguzi Mkuu. Alitaja michezo itakayoshindaniwa kuwa ni soka na vishale ambayo itashindanisha timu za wanaume na netiboli wanawake.

Michezo ambayo itashindaniwa na wanaume na wanawake ni kuvuta kamba, riadha, bao, karata, drafti na mbio za baiskeli. Shirikisho hilo limeomba viongozi wa klabu za michezo kuwapa umuhimu wa kwanza walemavu ambao wanauwezo wa kushiriki michezo hiyo.

“Tunaomba kama kuna watu wenye ulemavu ambao wanauwezo wa kushiriki kati ya michezo itakayoshindaniwa wapewe kipaumbele katika uteuzi wa timu,” alisema. Sululu alisisitiza klabu zote wanachama kuthibitisha michezo watakayoshiriki hadi Septemba 30 na kufika Tanga siku moja kabla ya mashindano kuanza.

Katibu huyo pia aliwakumbusha wanachama kulipa ada ya mwaka Sh 600,000 na 400,000 ya ushiriki kwa wakati kabla ya Septemba 30. Wakati huohuo Sululu alisema Mkutano Mkuu wa Shimiwi uliokuwa umepangwa mwezi huu umesogezwa mbele hadi baada ya mashindano ya Shimiwi.


Na: Anna Makange, Tanga

Monday, March 21, 2011

VIJIMAMBO VYA TANGA MIKONONI MWAKO SASA!!

Je una habari inayohusu Tanga, ambayo ungependa itolewe kwenye Blog hii ambayo inahusu mambo yote ya mkoa wa Tanga!!? Tutumie habari kupitia e-mail yetu ambayo ni ankomo25@yahoo.com

"LETTER TO MY FATHERS" POEM BY JANUARY MAKAMBA



This is a poem written and delivered by January Makamba, MP for Bumbuli, at Pen&Mic (a trimonthly literary, poetry and live music event) in Dar es Salaam, February 6th, 2011. The poem is an appeal for a new generation of leadership in Tanzania

MDUMANGE HUWOOOO!!

Thursday, March 17, 2011

LIBENEKE JIPYA MTANDAONI!!

MAZOEZI YA MISS TANGA CITY CENTRAL 2011 YAZIDI KUPAMBA MOTO!




MISS TANGA CITY CENTRAL 2011 ITAFANYIKA SIKU YA PASAKA (aliyevaa top nyekundu wa kati ndio mwalimu wa show)

UNAIKUMBUKA HII!!? ENZI HIZO MABAUNSA WA TANGA

Washindi wa shindano la kumtafuta Mt. Tanga enzi hizo. Kutoka kushoto Emmanuel Kaini (Mshindi wa pili)...Kaini amewahi kuwa maarufu sana kwa uchezaji filamu za kibabe. Ikiwa ni pamoja na UNGA ADUI, SHAMBA KUBWA na nyingine nyingi. George Adolf (Mshindi wa kwanza) na Maxwell Masabo (mshindi wa tatu)

Wednesday, March 16, 2011

MH. NUNDU ALIPOTEMBELEA BANDARI YA TANGA

Mbunge wa jimbo la Tanga mjini na pia waziri wa Uchukuzi Mh. Omari Nundu (Kushoto) na Mkurugenzi wa mamlaka ya usimamizi wa Bandari nchini (TPA) Bw. Ephream Mgawe, wakisiliza wafanyakzi wakitoa malalamiko yao juu ya ufanisi wa kazi za Bandari ya mkoani Tanga

Wafanyakazi wa Bandari ya Tanga wakiwa makini wakimsikiliza Mh. Nundu

Mmoja wa wafanyakazi hao akitoa malalamiko yake juu ya Bandari hiyo ambayo. Mfanyakazi huyo alidai kuwa mamlaka ya mapato (TRA) mkoani Tanga imekuwa kikwazo kikubwa cha Bandari hiyo ishindwe kufanya kazi kwa kuwanyanyasa wafanyabiashara.

Picha zote na Mashaka Mhando

OFFSIDE TRICK LIVE NDANI YA PWEZA CLUB TANGA!

Tuesday, March 15, 2011

HAPPY BIRTHDAY MTOTO REHEMA SWEDY MKWABI!

Ujumbe kutoka kwa mama mzaa chema Allice Joe Mkwabi (Pichani) kwenda kwa mtoto wake kipenzi Rehema.......

"U hv alwayz made me proud. My blessin r alwayz wit u.may god blec wit ol u desire,happy birth princess.am proud to hv u as my daughter! Lov frm mom, Luqman,granny and otherz"

Keki ambayo mtoto Rehema alikula pamoja na familia yake. Anko Mo Blogspot inakutakia maisha mema na marefu. Mungu akubariki sana Rehema, pamoja na familia yako yote.

TANGA LIFE NI MAJI SAFI YA KUNYWA KUTOKA TANGA!

Hivi karibuni katika pita pita zangu, nikakutana na maji haya ya TANGA LIFE. Binafsi nilifarijika sana kuona mkoa wetu wa TANGA una maji yake ya chupa ya kunywa. Hapa kulikuwa kwenye semina fulani katika Hostel ya Mwekasu. Chupa za maji zilizokuwa hapo zilinywewa zote. Na mimi nikapewa moja ninywe. Maji yalikuwa safi sana. Kama upo Tanga yatafute maji haya uyanywe, na kama wewe unatarajia kuja Tanga, basi usiache kunywa maji haya ukifika.

Huu ndio ujazo wa chupa ya maji ya TANGA LIFE!

Monday, March 14, 2011

ROMA LIVE NDANI YA LACASA CHICA 'MR PRESIDENT'

OFFSIDE TRICK WAFANYA KWELI TANGA!

Kundi la muziki wa kizazi kipya kutokea Zanzibar linalojilikana kama Offside Trick limekonga nyoyo za mashabiki wake pale walipofanya show ya uhakika kunako klabu ya Pweza iliyopo jijini hapa. Show hiyo ambayo ilikuwa ya aina yake, ilihudhuriwa na watu wengi huku wakisindikizwa na msanii mkali wa zouk kutoka Tanga, Sudy G!

Akina dada hawa walijimwaga vya kutosha. Hapa kitu cha khanga tu.

Klabu ya pweza ilikuwa haitoshi.

Vijana wa Offside Trick wakitoa burudani kwa mashabiki wao.

Masele a.k.a Ahmada alikuwepo kutoa burudani pia.

Thursday, March 10, 2011

MAZOEZI YA MISS TANGA CITY CENTRAL MOTO!

Warembo wa kitongoji cha Miss Tanga City Central wakiwa katika mazoezi kunako klabu Pweza iliyopo chuda relini. Kitongoji hicho ambacho ndio kimefungua pazia la mazoezi jijini hapa, kimejitapa kutoa mshindi kwa mwaka huu. Mbio za mashindano ya kumsaka mnyange wa Miss Tanga 2011 zimeanza hivi karibuni huku taji hilo likishikiwa na Anna Kiwambo ambaye ni Miss Tanga 210. Miss Tanga 2011 inaandaliwa na kampuni ya New Face Entertainment.

Mwalimu wa kitongoji cha Miss Tanga City Central bibie Mariam Bandawe.

Kitongoji cha Miss Tanga City 2011 kinaandaliwa na kampuni ya Green Apple Entertainment chini ya bibie Aisha Salim mwenye nywele ndefu pichani- akiwa na mwalimu wa dansi kwa warembo bibie Amina. Miss Tanga City inaletwa kwenu kwa udhamini wa Aurora Security, Madam Hair Dressing Saloon, J Pal, Amani Spares, na Anko Mo Blogspot....

Sunday, March 6, 2011

SHOW YA ROMA FUNIKO BOVU TANGA!!

Ile show ya msanii nguli wa hip hop kutokea Tanga R.O.M.A iliyofanyika kunako Club Lacasa Chica imekuwa gumzo jijini hapa baada ya msanii huyo kuzikonga nyoyo za mashabiki wake kwa kiwango cha juu. Show hiyo iliyopewa jina la NARUDI NYUMBANI PARTY, ilisindikizwa na wasanii wengine kama Belle 9 pamoja na Young D ambao nao walitoa burudani ya hali ya juu.

Roma akiwarusha wakazi wa jiji la Tanga alipokuja kuwashukuru kwa kumfikisha alipo sasa.

Warembo wa kitongoji cha Miss Central walikuwepo na walipita kuwasalimia mashabiki.

Msanii Belle 9 akiimba jukwaani kwa hisia kali kuhakikisha anawapa burudani mashabiki wake.

Mc wa show alikuwa Rass Bizzle kutoka Nyakubi Inc....

Vijana wa Town Boys walikuwepo. Na hapa kitu cha kiduku pale kati.

Jha, jha, jha.....Tayana alikuwepo. Kaa tayari, video za show nzima inakuja.


Thursday, March 3, 2011

NI ROMA IJUMAA HII NDANI YA CLUB LACASA CHICA!!

Msanii nguli wa hip hop anayetokea Tanga, ROMA atapiga show ya kuwashukuru wana wa TANGA wote kwa kumpa kampani toka alipoanza game mpaka kufikia leo. Show hiyo iliyopewa jina la NARUDI TANGA PARTY itafanyika Club Lacasa Chica kwa kiingilioa cha 4000/=. Roma atasindikizwa na Belle 9 pamoja na Young D. Tukutane hapo!

Wednesday, March 2, 2011

MPIGIE KURA TOP C SASA

Mpigie kura Top c awe msanii mpya anayechipukia kwenda namba 15747. Sehemu ya kuandikia ujumbe wako unaanza kuandika V125 kisha unatuma kwa namna 15747

Msanii mpya anayechipukia ::

Bob Junior
Sajna
Linah
Sam wa ukweli
Top C V125


Mpigie tena kura Top c ili wimbo wake 'Ulofa' uwe wimbo bora wa Zouk/Rhumba kwenda namba 15747. Sehemu ya kuandikia ujumbe wako unaanza kuandika Y181 kisha unatuma kwa namna 15747. Au kupiga kura kwa njia ya Internet BONYEZA HAPA


Wimbo Bora wa Zouk/Rhumba ::

Sina Raha -Sam
Ulofa- Top C Y181
Nabembelezwa - Barnaba
Bado Robo Saa - Amini
Bora Nikimbie -Linah

KUTANA NA MARAFIKI WENGI KUTOKA TANGA!


CHAT NA MARAFIKI WA TANGA BONYEZA HAPA


Ukiingia humo, unabonyeza mahala palipoandikwa CHAT WITH GROUP.....ipo pembeni. Furahia chat na MARAFIKI WA TANGA sasa!!!!!! ( hakikisha umefungua facebook yako kwanza)

Tuesday, March 1, 2011

ROMA/BELLE 9/ KUWASHA MOTO JIJINI TANGA IJUMAA HII!


Msanii wa Kizazi kipya Ibrahim Mussa a.k.a Roma anatarajia kuwasha moto mjini Tanga kuwashukuru wakazi wa mkoa huo kwa kuweza kumuunga mkono katika kazi yake ya sanaa ambayo amekuwa akiifanya.

Akizungumza na blog hii, mratibu wa tamasha hilo lililopewa jina la 'Narudi Nyumbani Tanga, Bw. Nickson Amos alisema kuwa litafanyika katika ukumbi wa La Gland la Casa chica Ijumaa ya tarehe 4.03.2011.

"Kweli Roma atafanya tamasha lake binafsi ambalo anatarajia kusindikizwa na Belle 9 na Young D hivyo wakazi wa Tanga waje kwa wingi kumuunga mkono.

Aliongeza kuwa lengo la tamasha hilo kuwashukuru wakazi wa Tanga kwa kuweza kumuunga mkono tokea ameanza kazi zake.